Home » » Rais Kikwete azindua mradi wa umeme Ludewa

Rais Kikwete azindua mradi wa umeme Ludewa

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ludewa,Mh. Filikunjombe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa.Rais Kikwete alizindua mradi wa Umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utoonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya Maua kutoka kwa mtoto Chipukizi wakati walipowasili mkoani Iringa.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiwa na Mbunge wa Ludewa Mh Filikunjombe na Mwenyekiti wa CCM Iringa muda mfupi kabla ya kuzindua mradi wa Umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Katibu Mkuu Kiongozi,Mh Philemon Luhanjo akisalimia wananchi wa Mawengi wakati wa mkutano wa hadhara kufuatia uzinduzi wa mradi wa umeme wa Luwawa
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Mawengi wakati wa mkutano wa hadhara kufuatia uzinduzi wa mradi wa umeme wa Luwawa.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akisalimia wananchi wakati akiwa njiani kuelekea Mawengi, Ludewa Kuzindua mradi wa umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utaonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Wanafuzi wa shule za msingi katika wilaya ya Ludewa,Mkoani Iringa ambako yupo kwa ziara ya kikazi na kuzindua wa mradi wa umeme wa Luwawa.
Wananchi wa Ludewa wakimshangilia Rais Dkt. Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia.
Rais Kikwete akioneshwa sehemu ya maporomoko ya mradi wa umeme wa Lumama
Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya Mradi huo wa Umeme kutoka kwa Mtaalam wa Mradi huo.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akizindua na kukagua mradi wa Umeme wa Lumama kijiji cha Mawengi, Ludewa, utaonufaisha wananchi wapatao 10,000 katika vijiji vya Lupande, Mawengi na Madunda
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishukuru kwa zawadi ya kuku aliyopowa kijijini Mawengi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa umeme.
Rais Kikwete akimshukuru Meneja wa Mradi wa Umeme wa Lumama Bi Alice Michelezi wa taasisi ya Acra baada ya kupokea risala yake aliyoitoa kwa Kiswahili fasaha na kumfurahisha kila mtu.
Rais Kikwete akipata mapokezi makubwa kijijini Mawengi.
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na watawa wa Kanisa Katoliki la Mawengi mara baada ya kuwasili hapo.
Picha Zote na Ikulu.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. PICHA NA HABARI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger