Home » » JUMA NATURE ALIPOTEKA HISIA ZA MASHABIKI KATIKA TAMASHA LA STR8 MUZIK LILILOFANYIKA DODOMA

JUMA NATURE ALIPOTEKA HISIA ZA MASHABIKI KATIKA TAMASHA LA STR8 MUZIK LILILOFANYIKA DODOMA

Katika Tamasha La STR8 MUZIK lililofanyika Mkoani Dodoma Jana Jumamosi Msanii Juma Nature alitokea Kuwa Kivutio Kikubwa sana Kwa Mashabiki ambapo walimtaka Aendelee Kutumbuiza Jukwaani
Msanii wa Kizazi Kipya Juma Nature akiwa na Kundi lake la TMK Wanaume Halisi wakifanya Makamuzi Katika Tamasha la STR8 muziki lililofanyika Jumamosi katika viwanja vya royal village mjini Dodoma.
Juma Nature aka Kiroboto akishusha mistari ya moja ya nyimbo zake za zamani lakini zilibamba mbaya katika tamasha hilo la STR8 muzik ndani ya viwanja vya royal village mkoani Dodoma
Msanii Wa Kizazi Kipya Mansu Lii Akiwa Kwa Steji wakati alipopanda kumpa tafu Juma Mchopanga aka J MO katika tamasha la STR8 Muzik lililofanyika Jumamosi katika Viwanja Vya Royal Village mjini Dodoma.
Mashabiki wakiwa wamepandisha mzuka wakati Juma Nature akiwa Stejini akifanya Makamuzi katika tamasha la STR8 Muzik lililofanyika katika viwanja vya royal village mjini Dodoma.
...............................................................
Msanii Juma nature alitokea kuvuta hisia za mashabiki wengi pale alipoanza kuimba nyimbo zake za zamani na mashabiki kutaka Juma Nature kuendelea kubaki stejini akitoa buradani.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. PICHA NA HABARI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger