Home » » TASWIRA ZA MAONYESHO YA PICHA YA "AMRIK"

TASWIRA ZA MAONYESHO YA PICHA YA "AMRIK"

 Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Bw. Navroz Lakhani ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maonyesho hayo akizungumza machache katika hafla ya ufungaji wa maonyesho hayo.
Pichani ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu akisoma hotuba kwa wageni waalikwa katika maonyesho ya Picha yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya "AMRIK" yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Brazil, Taasisi za nchi za Kiarabu  na Aga Khan. Ambapo Balozi huyo amewapongeza walioshiriki maonyesho hayo. Maonyesho hayo yenye lengo la kuhamasisha ushirikiano kati ya Wabrazil na Waarabu yalitarajiwa kufanyika wiki iliyopita lakini yakaahirishwa kufuatia ajali ya kuzama kwa Meli ya MV SPICE ISLANDER iliyotokea huko Zanzibar.Katikati ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu na Kushoto ni Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Bw. Navroz Lakhani.
Kutoka kushoto pichani ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu, Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz na Makamu wa Balozi Bw. Ronaldo Vieira wakisikiliza hotuba kutoka kwa Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan (hayupo pichani).
Afisa Ubalozi Lucy Mwambungu akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa siku nyingi wa michezo ya Kuigiza maarufu kama Sinta pamoja na Makamu wa Balozi wa Brazil nchini Ronaldo Vieira.
Mke wa Balozi wa Brazil nchini Mama Luz akibailishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa.
Balozi wa Marekani nchini Alfonso E. Lenhardt akiangalia picha zilizokuwa zimetandazwa katika maonyesho hayo.
 Pichani juu na chini ni wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali nchini, Taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali wakifuatilia picha zilizokuwa zikionyeshwa katika maonyesho hayo jijini Dar es Salaam.
 Pichani Juu na Chini ni miongoni mwa wadau mbalimbali kutoka sehemu na Idara Tofauti za ndani na nje ya nchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla hiyo ya maonyesho ya picha yanayoelezea ushirikiano wa nchi  ya Brazil na zile za kiarabu katika nyanja mbalimbali.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. PICHA NA HABARI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger