Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya "AMRIK" yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Brazil, Taasisi za nchi za Kiarabu na Aga Khan. Ambapo Balozi huyo amewapongeza walioshiriki maonyesho hayo. Maonyesho hayo yenye lengo la kuhamasisha ushirikiano kati ya Wabrazil na Waarabu yalitarajiwa kufanyika wiki iliyopita lakini yakaahirishwa kufuatia ajali ya kuzama kwa Meli ya MV SPICE ISLANDER iliyotokea huko Zanzibar.Katikati ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu na Kushoto ni Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Bw. Navroz Lakhani.
Kutoka kushoto pichani ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu, Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz na Makamu wa Balozi Bw. Ronaldo Vieira wakisikiliza hotuba kutoka kwa Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan (hayupo pichani).
Mke wa Balozi wa Brazil nchini Mama Luz akibailishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa.
Balozi wa Marekani nchini Alfonso E. Lenhardt akiangalia picha zilizokuwa zimetandazwa katika maonyesho hayo.
Pichani juu na chini ni wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali nchini, Taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali wakifuatilia picha zilizokuwa zikionyeshwa katika maonyesho hayo jijini Dar es Salaam.
Post a Comment